Uandikishaji wa PHLpreK uko wazi!

Tangu ulipoanza mwaka 2017, PHLpreK umehudumia wanafunzi zaidi ya 10,000. Mwaka huu, mpango wa elimu ya awali ya bure na bora utahudumia zaidi ya wanafunzi 4,000 katika maeneo zaidi ya 160 katika Jiji lote! Tumejiandaa kuikaribisha familia yako katika mwaka mzuri kuwahi kutokea!

PHLpreK unapatikana kwa watoto wenye umri wa miaka 3 na 4 ambao wanaishi katika Jiji la Philadelphia. Huenda unastahiki ya kumuandikisha mtoto wako kwa ajili ya mwaka wa masomo wa 2021-22 wa PHLpreK ikiwa:

  • Mtoto wako atafikisha miaka 3 au 4 ifikapo Septemba 1, 2021
  • Wewe ni mkazi wa Philadelphia

Hakuna matakwa ya kipato au ajira.

Tazama orodha ya sasa ya mipango ya PHLpreK au piga simu 1-844-PHL-PREK ili kupata mpango wa bure na bora ulio karibu yako!

Unaweza kuwasiliana moja kwa na mpango wowote wa kushiriki ili kujiandikisha katika PHLpreK katika mpango wao. Iwapo unahitaji msaada, piga simu 1-844-PHL-PREK ili kupata taarifa zaidi kuhusu kuanza mchakato wa kutuma maombi.

Kujiandikisha, familia zitahitaji nyenzo zifuatazo:

  • Hati moja ya uthibitisho wa umri, kama vile:
    • Cheti cha Kuzaliwa,
    • Pasipoti halali ya Marekani,
    • Kadi ya hifadhi ya jamii,
    • Kumbukumbu za matibabu au za shule.
  • Hati moja ya uthibitisho wa makazi, kama vile:
    • Kitambulisho kilichotolewa na serikali au leseni ya udereva,
    • Kitambulisho cha mpiga kura,
    • Mkataba wa sasa wa upangaji au makubaliano ya upangaji,
    • Barua ya malipo ya Hifadhi ya Jamii.

Wasiliana na mpango unaopenda kushiriki kwa njia ya simu au barua pepe ili kuthibitisha kama wana nafasi na kujua jinsi ya kujaza nyenzo za kujiandikisha.

Watoa huduma ya PHLpreK watafuata miongozo ya afya na usalama ya mahali husika, jimbo na taifa.

PHLpreK ni mpango wa elimu ya awali ya bure na bora wa Jiji la Philadelphia ambao unawapa watoto msingi imara wa elimu yao. Ukiwa umefadhiliwa kwa Kodi ya Vinywaji ya Philadelphia, mpango wa PHLpreK unazisaidia familia katika Jiji zima la Philadelphia kupata fursa za elimu ya awali ya gharama nafuu na bora.

Pata taarifa zaidi kuhusu PHLpreK na jiandikishe leo

Tafuta mpango wa PHLpreK ulio karibu na wewe